Pishi la Kuku na Mchicha | Kula na Mashed Potatoes | Viazi vya Kuponda



Kupika ni ubunifu na kupika ni muunganiko wa vitu na viungo (spices), ile ujue ukiweka nini na nini vitaleta ladha ya namna gani.. Hapa nakuonyesha jinsi nilipika Kipande cha kuku na mchicha ambayo nilikula na viazi vya kuponda

Mlo wa mtu mmoja

MAHITAJI


  • Paja la kuku 
  • Mchicha fungu moja
  • Viazi mviringo 2 - Menya na kukata vipange vidogo dogo
  • Kitunguu Maji 1 - katakata
  • Kitunguu maji 1 - katakata
  • Punje za Kitunguu swaumu 3 -  twanga
  • Chumvia kiasi upendacho
  • Pilipili Manga 1/4 - kijiko cha chai
  • Karoti - moja katakata
  • Udaha / cayenne - just a pinch
  • Binzari ya Njano - 1/4 kijiko cha chai
  • Mafuta ya kupikia - 2 vijiko vya mezani
  • Maziwa fresh - vijiko 4 vya mezani

JINSI YA KUPIKA

  1. Kwanza anza na kuku katika moto wa kati. Katika chombo weka kuku, mafuta ya kula, chumvi, pilipili manga, kitunguu swaumu, kitunguu maji, binzari ya njano, karoti na maji kiasi kisha funika wacha ichemke ....baada ya dakika kama 6 hivi funua na geuza kisha ongeza maji kidogo kama yamepungua.. wacha iendelee kuchemka kwa dakika 10. Baada ya hapo ni tayari. 
  2. Toa kipande cha kuku tu katika chombo - weka kando kisha katika ile supu iliobaki wakati wa kupika kuku weka mchicha kiasha pika kwa dakika moja - ondoa na weka kando rudishia ile kuku na kufunika.
  3. Sasa kupika viazi - chemsha hadi viive na viweze kupondeka. Wakati wavichemsha weka black pepper, chumvi na mafuta kidogo au butter
  4. Vikiwa tayari chuja maji na anza kuviponda au kuvisonga ..... vikishakupondeka weka maziwa ili kupata ulaini mzuri. Baada ya hapo ni tayari kwa kula na ile kuku yetu. 

No comments:

Post a Comment

@chefkile