Jinsi ya Kupika Mchezo wa Ndizo Mzuzu na Nyama ya Ng'ombe



Mimi ni mpenzi sana wa kula ndizi mzuzu, ikiwa za kuchoma, kukaanga na mafuta au hata kuzichemsha. Mapenzi yangu hayo yamepelekea leo mie kuja na pishi hili zuri na nimeonelea ni vema nawe ulijue.

Chakula kwa watu 2

MAHITAJI 


  • Nyama ya Ng'ombe robo
  • Ndizi mzuzu mbichi 5 
  • Vitunguu maji 1 
  • Kitunguu swaumu punje 3 
  • Giligilani vijani vichache 
  • Rosemary vijani vichache 
  • Bay vijani vichache 
  • Chumvi - kwa kiasi upendacho 
  • Olive oil kijiko cha mezani kimoja 
  • Pilipili- kama watumia 
  • Karoti moja 
  • Pilipili manga 

JINSI YA KUPIKA 



  1. Kwanza chemsha nyama - sasa wakati wachemsha nyama weka chumvi, maji kwa kiasi, bay, rosemary, garlic na pilipili manga. 
  2. Angalia kiasi cha maji - lengo ni kupata supu ivo unaweza kuongeza maji 
  3. Ichemke hadi kuiva ndipo uweke vitunguu maji na swaumu pamoja na ndizi kisha acha ichemke na kuiva kwa dakika takribani 15, kishi weka karoti na ivisha tena kwa dakika 4 au 5. Baada ya hapo mchemsho upo tayari kwa kuliwa na ni mlo kabimili. Ukiwa unapakua ndio mda wa kuweka vile vijani vya giligilani.

No comments:

Post a Comment

@chefkile