Jinsi ya Kutengeneza Tambi na Kuzipika


Siku moja nikiwa naagalia Tv, nikaona watu wa Vietinum wanapata fresh pasta ambazo wanaziandaa wenyiwe. Nami nikafanya kujiandalia na kupata matoke mazuri sana. Nikaona kwa kupata kitu kizuri ni muhimu na wengine wajue nami naweka katika maandishi kama hivi.

Mlo wa kutosha watu 2

MAHITAJI KWA TAMBI ( FRESH PASTA) 


  • Unga wa ngano 1/4 kg 
  • Mayai 2 ya kienyeji  
  • Mafuta ya Olive oil vijiko 3 vya mezani 
  • Chumvi kijiko 1 cha mezani 

MAHITAJI KWA SAUCE 



  • Minofu ya kuku ( kidari kimoja kinatosha - chemsha na chumvi tu kawaida) 
  • Njegere - 1/4 kg zichemshe ziive 
  • Tomato paste vijiko 3 vya mezani 
  • Chumvi kwa kiasi utumiacho 
  • Mafuta ya kupikia olive oil au mafuta yoyote ya mimea vijiko 3 
  • Nyanya kawaida 3 ( menya na kuzikata kata) 
  • Vitunguu maji 2 ( Menya na kuvikata kata) 
  • Vitunguu Swaumu - punje 3 ( menya na kuviponda ponda) 
  • Mahanjumati Masala ( ile spice mix ya ChefKile) Kijiko 1 cha chakula 

JINSI YA KUANDAA 



  1. Hatua ya kwanza ni kuandaa unga wa pasta. Chukua bakuli weka unga na vunja mayai yako mawili weka na chumvi kisha anza kuuchanganya alafu ongeza na yale mafuta. Mchanganyiko hautakuwa laini utabaki mgumu mgumu, funga katika nailoni na acha kwa dakika zisizopungua 20 ( ni vema ukaweka katika friji). 
  2. Sasa unga ukiwa unaendelea kufikia kiwango kwa kuwa pembeni ni muda wa kuandaa sauce ya pasta yako. 
  3. Weka chombo chako cha kupikia katika moto na mafuta vijiko vitatu, mafuta yakipata moto weka vitunguu ivisha kidogo kisha weka kitunguu swaumu na endelea kuivisha. 
  4. Vikiwa vinabadirika rangi ongeza zile nyanya, chumvi na ile mahanjumati masala ivisha kabisa na nyanya zikiwa zinakaribia kuiva ndipo uweke ile tomato paste kisha ivisha dakika 3 zaidi na uweke njegere na minofu ya kuku.
  5. Ukiweka njegere na minofu ya kuku ongeza maji kidogo, kisha acha ichemke kwa dakika 3 au 4. Ikiwa Tayari weka kando turudi kwenye pasta sasa. 
  6. Ukiangalia ule unga baada ya hizo dakika 20 au zaidi utakuta umebadirika rangi kuwa kama umeshikana zaidi - Ukande tena kidogo kisha tengeneza mabonge kama ya chapati na andaa na unga mkavu zaidi. Maaana huwa unahitajika sana. 
  7. Anza kusukuma kama chapati hivi ila tumia unga mwingi ili iwe kavu kavu - Ukishapata ile duara viringisha - kisha kata vipande kwa kufuata mviringisho ule wa duara na utapata vitu mfano wa tambi kama tulivyozoea 
  8. Fanya hivyo kwa zote - kisha pasha maji mto weka na chumvi kidogo yakichemka weka tambi zako kwa dakika 3 tu kisha toa na uachanganye na ile Sauce sasa... alafu wacha vipikike kwa pamoja kwa dakika 3 -4 . Baada ya hapo pishi lako lipo tayari. Furahia pishi maana najua ni tamu sana ingawa linachukua muda kuandaa

No comments:

Post a Comment

@chefkile