Jinsi ya Kupika Mkate Kwa Ngano Dona ( Unga wa Atta)


Ikiwa uko nyumbani na una muda wa kutosha basi ni vizuri sana ukajiandalia mkate wako mwenyewe. Kuna faida nyingi sana unapojipikia mkate wako zaidi ikiwa ni kiafya. Hapa nimeona ni vema nikushirikishe namna ya kuupika maana ni rahisi sana.

MAHITAJI


  • Unga wa ngano atta nusu na robo ( atta - ni unga wa ngano isiyo kobolewa)
  • Maziwa robo lita 
  • Amira kijiko kimoja na robo cha mezani 
  • Maji vugu vugu kwa kukandia 
  • Chumvi robo kijiko 
  • Sukari vijiko 3 vya mezani 

 JINSI YA KUPIKA 



  1. Anza na kuyeyusha amira katika maji ya uvugu vugu. Ivo changanya maji , sukari na amira kisha acha kwa dakika 5. Ikiisha kuyeyuka na kuumuka ndio weka katika chombo pamoja na unga, chumvi, na maziwa kisha kanda kwa dakika kumi. Ikiwa unga ni mgumu ndipo utaongeza maji kidogo tu kuuweka katika hali ya ulaini kiasi ila sio tepe tepe.
  2. Unga ukiwa tayari acha uumuke kwa dakika 20, kisha uukande tena na kuweka katika chombo utachopikia; acha uendelee kuumuka tena kidogo. Pasha jiko moto , na ukiona unga umeumuka kiasi ndipo uuweke mkate wako na kuuoka kwa dakika 30 hadi 45 ikitegemea na joto la jiko lako.
  3. Kujua kama mkate umeiva chomeka kisu katikati hadi chini kisha chomoa kama kikitoka bila kuwa mkate umegandia basi ujue umeiva vema. Acha upoe kwa muda kidogo alafu ndio ufurahie mkate wako

No comments:

Post a Comment

@chefkile