Kupika Samaki na Tambi



Hili ni moja ya mapishi marahisi sana na huwa nafurahia sana kula mlo huu nyakati za mchana. 

Chakula cha watu 2

MAHITAJI 

Kwa ajili ya samaki utahitaji

  • Samaki kiasi ya nusu kilo 
  • Pilipili manga 1/2 ya kijiko cha chai 
  • Chumvi 1/2 ya kijiko cha chai 
  • Maji ya limao moja 
  • Mchanganyiko wa majani (mixed herbs) huwa inauzwa katika supermarkets 
  • Mafuta ya kula vijiko 4 vya chakula - mafuta ni kwa ajili ya kukaanga samaki Kwa ajili ya Tambi 
  • Tambo aina yoyote kiasi ya 1/4kg 
  • Mafuta ya kula kijiko cha chai ( zaidi ikiwa ni olive oli ni nzuri zaidi) 
  • Maziwa fresh yenye cream robo lita 
  • Chumvi nusu kijiko cha chai 
  • Kitunguu maji kimoja - kikatwe katwe 
  • Kitunguu swaumu punje 2 zimenywe na kupondwa pondwa 

 JINSI YA KUANDAA 



  1. Tunaanza na Samaki - kwa jinsi alivyo kata kwa ubapa ubavu ule wa juu na wa chini kupata vipande viwili. Kisha mnyunyuzie chumvi, pilipili manga, mchanganyiko wa majani na maji ya limao kisha acha kwa dakika 5 tu. 
  2. Baada ya dakika 5 weka kikaangio katika moto wa washani sio mkali pia weka mafuta - waweza dhani mafuta ni madogo la hasha ni kiasi hicho hicho. Kikaangio kiwe kipana ili uweze weka samaki wote wawili kwa kuanza na upande ile wenye ngozi... 
  3. Ivisha upande huo kwa daki 6 kisha geuza upande mwingine kwa dakika 3. Alafu epua na uwaweke kando kuwakiwa wanapumzika ( kitaalamu ni resting while its cooking slowly and getting tender) 
  4. Sasa Twende na Tambi - chemsha maji katika chombo weka chumvi kidogo , yakiwa yamepata moto wa kutosha ndipo uweke hizo tambi - kawaida tambu huchukua dakika 5 hadi 15 inategemea na aina ya tambi. Hivyo zikisha kuwa na ulaini wa kuonyesha kuiva epua na kuzitoa katika maji moto na zimwagie maji baridi kabisa na kuyachuja. Kumwagia maji kunafanya zisishikane. 
  5. Weka chombo kingine katika moto na mafuta kidogo kisha anza kukaanga vitunguu swaumu kwa nusu dakika kisha weka vitunguu maji, ongeza chumvi kidogo pia. Ivisha kwa dakia 2 au 3 ndipo uweke maziwa na endelea kukoroga na maziwa yakiwa yanachemka na kupungua kidogo uweke tambi na kuchemsha kwa pamoja kwa dakika 3 au 4. Baada ya hapo pishi lipo tayari, pakuwa tambi zako katika sahani na weka kipande cha samaki na waweza weka urembo wa chakula kwa kuweka hapo kipande cha ndimu au limao na majani ya giligilani.

No comments:

Post a Comment

@chefkile