Kupika Chapati za Kijani



Hii ni chapati ya kawaida kabisa ila mimi nimeiita chapati ya kijani baada ya kuongeza kiungo kimoja na kuifanya chapati ya afya zaidi.

Chapati 2

MAHITAJI


  • Unga wa ngano 1/4 kg 
  • Chumvi nusu kijiko cha chai
  • Mafuta ya kupikia vijiko 5 vya chakula 
  • Mchicha fungu moja ( uoshwe vizuri na kukatwa katwa) 
  • Maji nusu kikombe 

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA 



  1. Kwanza anza na mchicha unachofanya ni kuuweka katika blenda na maji kidogo kisha unasaga kwa pamoja ili upate yale maji ya kijani kutoka katika mchicha. Kisha wachuja na kuweka yale maji ya kijani kando 
  2. Sasa chukua chombo cha kukandia unga wa chapati - Weka unga, chumvi kidogo na sasa katika kuukanda badala ya kutumia maji ya kawaida hapa watumia yale maji yaliyotokana na mchicha. 
  3. Kanda unga hadi kufikia kiwango kile kile cha unga ufaao kupika chapati - Hapa nimeandika nikiamini unajua kupika chapati ila katika hii ni kuwa tumeongeza rangi. 
  4. Baada ya hapo kata katika mafungu ya kutosha chapati moja kwa idadi ya unga kutoa na kuzipika chapati zako Ni hivyo tu na ni rahisi sana na unakuwa umepaata chapati yenye afya kabisa maana virutubisho vyote vilivyopo katika mchicha navyo umepata.

No comments:

Post a Comment

@chefkile