Aina hii ya supu niliwahi ona bibi yangu anaipika miaka ya 90 na alikuwa anapika kwa ajili ya mama aliyekuwa mzazi wakati huo. Nikabahatika kuonja na niliipenda sana. Sasa nikiwa katika miaka hii ya utu uzima nikakumbuka mahitaji yake na namna ya kuipika. Nilijaribu mara kadhaaa na baadae nikaipatia sana. Hapa nitakwenda kukushiharikisha na wewe pishi hili zuri.
Supu ya kutosha watu 5
MAHITAJI
- Nyama ya ng'ombe 1/2 kg ( nyama iliyosagwa na isiwe na mafuta mengi)
- Pilipili manga kijiko 1 cha chai
- Siagi ya Butter vijiko 3 vya mezani
- Maziwa fresh 1/2 lita ( yapashe moto)
- Vitunguu maji 2 ( menya na kukata kata)
- Kitunguu swaumu punje 4 (menya na kuviponda ponda)
- Chumvi kiasi upendacho
- Unga wa ngano vijiko 2 na nusu - kijiko cha mezani
- Mchanganyiko wa viungo vya mimea kijiko 1 cha mezani (mixed herbs)
- Pilipili kama ni mtumiaji
JINSI YA KUIPIKA SUPU
- Kuchemsha nyama - Chemsha nyama katika chombo weka chumvi tu na usiweke maji. Wacha ichemke hadi ianze kukakuka ndipo uongeze maji. Unapoongeza maji weka na ile mixed herbs pamoja na pilipili manga vichemke pamoja hadi nyama itakapokuwa imeiva.
- Baada ya nyama kuwa tayari chukua chombo kingine kwa ajiri ya supu. Weka katika moto na uweke yale mafuta ya butter yakiyeyuka weka vitunguu maji na swaumu; ivisha kidogo tu na uweke ule unga wa ngano na uendelee kukoroga hadi unga uwe unaelekea kubadiri rangi kidogo. ( ikiwa unga umekuwa mkavu sana unaweza ongeza mafuta ya kawaida kidogo)
- Baada ya unga kuwa na rangi kidogo weka ile nyama na uendelee kuikoroga zaidi ikiwa inakuwa kavu ndio muda wa kuongeza yale maziwa huku unakorogoa itaanza kuwa laini kama uji endelea hadi kufikia kiasi upendacho.
- Sasa mda huo ndio uangalie kama chumvi inatosha na kama unapenda pilipili ndio unaweza kuongeza kidogo. Acha ichemke kwa dakika 5 zaidi. Baada ya hapo supu ipo tayari na inafaa kwa kula na chochote kile
No comments:
Post a Comment