Mara nyingi ndizi huwa twazipika na nyama au utumbo; sasa hapa nakushikirikasha katika pishi la ndizi pamoja na samaki na pronzi. Ni pishi ambalo tamu sana na mara utakapolipika basi huwezi jututia kabisa.
Pishi la watu 4
MAHITAJI
- Ndizi mshare - ( za kutosha watu watu 4 kadiria kwa jinsi upikavyo) menya na kuzikata vipande
- Samaki (king fish) 1/2 kg ( msafishe na kumkata vipande)
- Prozi 1/4 ( wasafishe vizuri)
- Chumvi kwa kiasi upendacho
- Mchanganyiko wa viungi vya mimea ( mixed herbs) kijiko 1 cha mezani
- Tui zito la nazi 1/4 ltr
- Vitunguu maji ( menya na kukatakata)
- Vitunguu swaumu punje 4 ( menya na uviponde ponde)
- Mahanjumati Masala kijiko 1 na 1/2 cha mezani
- Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya mezani
- Binzari 1/2 kijiko cha chai
- Karoti 2 ( menya na kuzikata kata vipande)
JINSI YA KUPIKA
- Cha kwanza unazibandika ndizi - weka maji kidogo tu, chumvi, mixed herbs, mafuta ya kupikia. Kisha acha zichemke kwa dakika 10 - angalia kama ndizi zinaelekea kuiva - kama bado unaweza ongeza maji kama zinahitaji. Weka na ile binzari wakati huu. Achaa zichemke kama dakika 3
- Sasa weka zile samaki na pronzi, vitunguu maji na swaumu pamoja na ile mahanjumati masala. Kisha acha vichemke tena kwa pamoja kwa dakika chache huku ukiangalia visiive hadi kulainika sana.
- Vikiwa katika hali ya utayari weka lile tui la nazi kiasha anza kukoroga kwa umakini bila kuharibu ili tui la nazi lisikatike.. likianza kuchemka tena onja chumvi kama haitoshi waweza ongeza na kuacha ichemkie dakika 2 au 4; Pishi lako lipo tayari.
No comments:
Post a Comment