Jinsi ya Kupika Mchuzi wa Kuku Mtamu


Mboga ya kuku yapendwa sana sehemu mbali mbali na ina namna nyingi sana za upikwaji wake. Sasa hapa nitakuonyesha namna ambayo unaweza ipika mboga ya kuku na kuwa tamu sana na itakayofaa kwa kula na vyakula mbalimbali kama wali, chapati, viazi , ndizi nk.
Kupika mboga ya kutosha wat 6

 MAHITAJI 


  • Kuku mmoja wa 1 kg 
  • Vitunguu maji 3 ( menya na kukatakata) 
  • Nyanya 5 zilizoiva vizuri ( menya na kuzikata kata au kuzisaga na machine) 
  • Mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi kijiko 1 cha mezani ( zilizopondwa pondwa)
  • Mchanganyiko wa viungo/Garam masala/Mahanjumati masala vijiko 2 vya mezani 
  • Mafuta ya kupikia vijiko 4 vya mezani 
  • Pilipili manga kijiko cha chai nusu 
  • Bilinganya moja iwe teketeke ( menya na kuikatakata vipande vidogo vidogo) 
  • Kijiko kimoja cha binzari njano ( kijiko cha chai) 
  • Chumvi kwa kiasi upendacho 
  • Majani machache ya bay 
  • Majani ya Giligilani kutosha kiganja cha mkono ( katakata upendavyo) 

JINSI YA KUPIKA PISHI HILI 



  1. Hatua ya kwanza ni kukatakata ile kuku vipande vidogo vidogo na kisha kuichemsha - Sasa katika kuchemsha inategemea na aina ya kuku kama ni wa kisasa basi utachemsha kidogo tu kama dakika 5; ila kama ni wa Kienyeji basi utachemsha kwa dakika 15 - 20 . Katika kuchemsha weka chumvi , majani ya bay na pilipili manga kidogo 
  2. Baada ya kuku wako kuwa tayari - Uchukue chombo utakachopikia sasa weka mafuta na acha yapate moto kiasi ndipo uweke vitunguu maji na viivishe dakika 2 ndipo uweke ule mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi na bilinganya kisha endelea kuivisha kwa dakika 3-5 ndipo uweke nyanya na ule mchanganyiko wa viungo au garam masala au Mahanjumati Masala endelea kuivisha kama itaonekana kavu kabla ya kuiva ongeza ile supu uliyochemshia kuku. 
  3. Pika nyanya hadi ziive kabisa kabisa hadi ziwe kama zinatengana na mafuta ikifikia hatua hiyo ndipo uweke vipande vya ile kuku bila mchuzi wake. Endelea kuvikoroga na nyanya ukiona vimeshikana vizuri ndipo uweke ile supu ya kuku kwa kiasi; pia onja chumvi na kama bado haijatosha unaweza kuongeza na kuacha ichemke kwa kama dakika 5 ila dakika moja kabla ya kuepua weka yale majani ya giligilani. 
  4.  Baada ya hapo pishi lako lipo tayari ni wewe kufurahi.

No comments:

Post a Comment

@chefkile